Walimu, wanafunzi na wazazi wanaendelea kusherehekea matokeo ya mtihani wa KCSE

  • | K24 Video
    5 views

    Walimu, wanafunzi na wazazi wanaendelea kusherehekea matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, KCSE huku waliosoma kwenye mazingira magumu wakiwashangaza wengi kwa kupata alama za juu. Kwa mfano, katika kaunti ya kakamega, pacha wamewashangaza wengi kwa kupata alama sawa japo ugonjwa wa mama yao mzazi umekuwa ukiwanyima usingizi kila kuchao. Shule ya upili ya wasichana ya bahari kaunti ya Kilifi nayo imeandikisha historia baada ya kuwa ya kwanza ya umma katika kaunti hiyo kuwa na mwanafunzi aliyepata alama ya. Matukio hayo likiwemo la mwanafunzi aliyepata alama ya a katika shule ya upili ya wavulana ya Alliance kuchinjiwa mbuzi na wazazi wake huko kapsabet