- 313 viewsDaktari wa Kipalestina Khaled al-Saedni anafanya kazi katika kitengo cha watoto cha hospitali ya Al-Aqsa Martyrs huko Gaza City. Daktari huyu, ambaye amefanya kazi katika hospitali hii kwa zaidi ya miaka 23, alipoteza mguu wake mwaka jana baada ya kujeruhiwa. Anasema alijeruhiwa na bomu katika kambi ya wakimbizi ya Al-Bureij katika miezi ya kwanza ya vita vya Gaza. Kutokana na matatizo yaliyotokana na maradhi ya kisukari, daktari huyu mwenye umri wa miaka 50 anasema, mguu wake ulikatwa. Lakini licha ya kutegemea kifaa cha kutembelea, daktari huyu wa watoto alisema amerejea kufanya kazi kuwahudumia watoto “katika fursa ya kwanza” aliyopata baada ya miezi kadhaa ya kufanyiwa upasuaji na kupata matibabu. “Nimepoteza mguu, namshukuru Mungu. Kuna watu familia zao nzima wamekufa shahidi – wake, watoto, wazazi na ndugu zao,” Saedni alisema, ana matumaini vita vya Gaza vitamalizika haraka. Israel ilianza mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya Gaza baada ya wapiganaji walioongozwa na Hamas kushambulia jamii za Waisraeli Oktoba 2023, na kuua watu 1,200 na kuwachukua mateka 250 kurejea nao Gaza, kulingana na hesabu za Isreali. Kampeni ya kivita ya Israeli tangu wakati huo imewauwa zaidi ya Wapalestina 46,500 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100,000, kulingana na wizara ya afya ya Gaza. Kampeni hiyo imewakosesha makazi watu milioni 2.3 na kuharibu eneo lote finyu la pwani. #ukandawagaza #daktari #khaledalsaedni #israel #mabomu #hamas #mateka #voa #voaswahili #kilema
Daktari
- 17 Jun 2025 - The victim, identified by locals as Moureen, was found lying in a pool of blood with her throat slit, prompting widespread shock and outrage in the quiet village.
- 17 Jun 2025 - Suba North Member of Parliament (MP) Millie Odhiambo has called for thorough investigations into the alleged suicide incident of arrested fisherman at Kipasi police post in Suba North constituency on Sunday.
- 17 Jun 2025 - The national government has launched a Ksh.60 million relief programme for Tana River residents affected by perennial flooding.
- 17 Jun 2025 - Ugandan President Yoweri Museveni has signed legislation that allows military tribunals to try civilians, parliament said on Monday, a move opposition leaders said violates a Supreme Court ruling.
- 17 Jun 2025 - Ugandan President Yoweri Museveni has signed legislation that allows military tribunals to try civilians, parliament said on Monday, a move opposition leaders said violates a Supreme Court ruling.
- 17 Jun 2025 - HELB recently blacklisted 71,806 loan defaulters.
- 17 Jun 2025 - The agency also issued prospective applicants of the way forward.
- 17 Jun 2025 - Only 2 nations beat Kenya, according to a new study.
- 17 Jun 2025 - DCI officer says Albert Ojwang's arrest was carried out on the orders of Mr Amin Mohammed.
- 17 Jun 2025 - Kenya and Finland have underscored the critical need to sustain international momentum behind Somalia’s peacebuilding process, particularly in light of the ongoing ATMIS drawdown and heightened regional sensitivities.