Skip to main content
Skip to main content

Msichana wa miaka 13 atoweka mtaani Karen

  • | Citizen TV
    7,586 views
    Duration: 2:48
    Familia moja jijini Nairobi inamsaka binti yao wa miaka 13 aliyetoweka mapema mwezi Septemba mwaka huu. Rahab Njoki Njuguna alitoweka alipokuwa katika jumba moja la kibiashara mtaani Karen. Kisa hicho kimefufua matukio yaliyoangaziwa na runinga ya Citizen ambapo jamaa anayejidai kuwa afisa mkuu wa polisi huko Kilgoris anazipigia simu familia za waathiriwa na kudai kuwaokoa waliotoweka kisha kuitisha pesa.