Shule ya wavulana ya Nakuru High yafungwa kufuatia rabsha za wanafunzi

  • | Citizen TV
    663 views

    Shule ya wavulana ya Nakuru Boys imefungwa kwa majuma mawili baada ya wanafunzi kuandamana na kuzua vurumai usiku wa kuamkia leo Inaarifiwa kuwa wanafunzi watatu walijeruhiwa kwenye vurumai hilo huku mali kadhaa ya shule ikiharibiwa. Mgomo huu ulianza dakika chache kabla ya saa tatu usiku, ambapo wanafunzi wamekuwa wakilalamikia usimamizi wa mambo kadhaa shuleni ikiwemo kutolewa kwa chai na hata kuhamishwa kwa mwalimu mkuu. Polisi walilazimika kuingilia kati kutuliza hali baada ya maandamano haya yaliyochukua zaidi ya saa nne