Vijana wapigwa risasi Baringo

  • | Citizen TV
    1,787 views

    Vijana wanne wanauguza majeraha ya risasi katika hospitali ya rufaa ya Baringo baada ya kudaiwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la Barwessa. Mauaji haya yakisababisha maandamano ya wakaazi wa eneo hili la Baringo Kaskazini, ambao walifunga barabara kulalamikia tukio hili. Inaarifiwa kuwa vijana hawa walijipata kwenye makabiliano ya polisi walipokuwa wakiingilia kati mzozo wa wizi wa mifugo. Sasa wakaazi hawa wanataka maafisa wanaodaiwa kuhusika kuhamishwa kutoka eneo hilo, wakiwashutumu kushirikiana na wezi wa mifugo.