Waziri Opiyo Wandayi azindua mpango wa usambazaji umeme kaunti ya Nyamira

  • | Citizen TV
    148 views

    Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amezindua rasmi mpango wa kuweka umeme mashinani maeneo ya Mugirango kaskazini, Nyamira Kusini na Kitutu Masaba. Kwenye mpango huo unaotekelezwa na shirika la REREC, zaidi ya familia 580 zinanuiwa kuunganishwa na huduma za umeme, kando na vibanda zaidi ya 50 vya kupima majani chai na maeneo mengine ya umma. Wenyeji na viongozi wa eneo hilo aidha wameomba serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi amepata huduma hizi bila ubaguzi, kwani maeneo mengi ya Nyamira Kaskazini yangali bila huduma hizi