Afueni ya wafanyakazi waliokuwa wakihudumu na USAID Kajiado

  • | Citizen TV
    105 views

    Wafanyikazi zaidi ya 200 ambao wamekuwa wakifanya kazi katika kaunti ya Kajiado chini ya mpango wa ufadhili wa USAID sasa wanaweza kushusha pumzi baada ya Gavana Jospeh Ole Lenku kuwaondolea hofu ya kupoteza kazi. Akizungumza kwenye hafla ya shukurani katika eneo la Dalalekutuk, Kajiado ya kati Gavana Lenku anasema licha ya mpango huo kuathirika, kaunti ya Kajiado itaendelea kuwapa kazi wafanyikazi hao ambao anasema watahamishiwa kwenye idara nyingine. Gavana Lenku pia akiwahimiza magavana wenzake kuweka mipango ya kunusuru ajira za wafanyikazi waliokuwa wakihudumu chini ya mpango huo,