- 542 viewsDuration: 1:33Wakazi wa eneo la Chemosit, kaunti ndogo ya Bureti kaunti ya Kericho wanaendelea kuutafuta mwili wa mtoto wa miaka minne aliyesombwa na maji ya mto Chemosit siku tano zilizopita. Viongozi wa eneo hilo waliungana na wakazi wakiitaka serikali ya kaunti kuimarisha mipango na miundombinu ya dharura ili kurahisisha shughuli za uokoaji pindi majanga yanapotokea. Kadhalika, waliwataka wakazi kuwa waangalifu zaidi kwa watoto, hasa katika msimu huu wa mvua .