- 8,486 viewsDarzeni ya wanajeshi wa Congo wamewekwa kizuizini huko Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, wakati mamlaka zikijiandaa kuwafungulia mashtaka wanajeshi wasiopungua 75 kwa kukimbia jeshini na vitendo vya ghasia dhidi ya raia, ikiwemo mauaji na uporaji. Kanda ya video kwenye mtandao wa kijamii iliyothibitishwa na Reuters Jumatatu (Februari 10) iliwaonyesha watu wakiwa na mavazi ya kiraia wakiingizwa kwenye Jela Kuu huko Bukavu. Mtazamaji katika kanda hiyo ya video aliwashutumu kuwa ni wanachama wa kikundi cha Cheetahs, kitengo cha jeshi la Congo, akisema “wanavuruga amani yetu.” Kuhusishwa kwa wafungwa katika video hiyo haukuweza kuthibitishwa na vyanzo huru. Reuters imethibitisha eneo hilo ni Bukavu kwa kulinganisha kuta za jela hiyo, lango kuu, miti yenye kuizunguka na milima na picha za satellite za eneo hilo. Wakati tarehe hasa ya kutolewa kanda hiyo ya video haikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru, ilikuwa imepakuliwa kabla ya Jumatatu siku ya kesi. Chanzo cha jumuiya ya kiraia huko Kavumu, mji ulioko kilomita 35 kaskazini mwa Bukavu, ameiambia Reuters kuwa wanajeshi waliokimbia waliwauwa watu 10, wakiwemo saba kati yao waliokuwa wameketi baa Ijumaa jioni. Ofisi ya mwendesha mahtaka ya jeshi ilisema wanajeshi hao wanakabiliwa na mashtaka ya kukimbia kutoka mstari wa mbele baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Nyabibwe, ulioko kilomita 70 kaskazini mwa Bukavu. Wanatuhumiwa pia kuhusika na ubakaji, mauaji, uporaji na uasi. (Reuters). #drc #congo #m23 #reels #voa
Wanaodaiwa kukimbia jeshini wawekwa jela kabla ya kesi kusikilizwa
- - Elimu bila mipaka ››
- 11 Aug 2025 - The British High Commissioner to Kenya, Neil Wigan is set to depart Kenya at the end of August marking an end to his 2 year tenure at the position.
- 11 Aug 2025 - Police in Eldoret have commenced investigations into an incident where a man received a parcel with three human fingers enclosed with six bullets.
- 11 Aug 2025 - Police in Eldoret have commenced investigations into an incident where a man received a parcel with three human fingers enclosed with six bullets.
- 11 Aug 2025 - Deputy Inspector General (DIG) of Police Eliud Lagat argues that the decision on whether to charge him over the death of blogger Albert Omondi Ojwang lies exclusively with the Director of Public Prosecutions (DPP) and not the courts.
- 11 Aug 2025 - The video widely shared on TikTok claims that the ’23-year-old’ was attacked during a performance.
- 11 Aug 2025 - The exposé contained footage allegedly showing minors being recruited into commercial sex work in Mai Mahiu
- 11 Aug 2025 - The nutrition survey indicates at least six million Kenyans are unable to afford essential food and non-food expenditures.
- 11 Aug 2025 - The ticketing malady witnessed in the ongoing CHAN 2024 competitions in Kenya has attracted censures from political leaders as many question the transparency of allowing football fans to secure tickets.
- 11 Aug 2025 - The clip of the assault went viral over the weekend.
- 11 Aug 2025 - "I am extremely sorry to be leaving Kenya after a whirlwind two years," Wigan said.