- 259 viewsDuration: 1:09Wizara ya Elimu imesitisha mgao wa karo kwa shule 29 nchini. Waziri wa Elimu Migos Ogamba ameiambia kamati ya bunge la kitaifa kuhusu elimu kwamba uchunguzi bado unafanywa kubaini iwapo shule hizo zinafaa kupokea mgao kabla ya kujumuishwa tena kwenye orodha. Ogamba amejibu haya kufuatia wasiwasi wa wabunge kuhusu fedha za kutosha shuleni, baada ya waziri kusema kuwa wizara yake ina uhaba wa shilingi bilioni 3.2.