- 31,339 viewsDuration: 15sTazama wakati mwenyekiti wa INEC, Jacobs Mwambegele alipomtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Mshindi wa kura za urais Tanzania. - Samia alipata kura milioni 31,913,866 kati ya kura 32,678,844 zilizopigwa. Hii ikiwa ni takriban 97.6 ya kura zote. Kumekuwa na maandamano nchini Tanzania tangu Oktoba 29 siku ya uchaguzi mkuu, vijana wakipinga uchaguzi huo. - Chanzo cha kidiplomasia kimeiambia BBC kwamba kuna ushahidi wa kuaminika kwamba angalau watu 500 wameuawa katika makabiliano hayo ya siku tatu katika miji ya Dar es Salaam , Dodoma, Arusha. - Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Thabit Kombo amesema Serikali haiwezi kuthibitisha idadi ya watu waliouawa kufuatia makabiliano baina ya vyombo vya usalama na waandamanaji. - Vile vile, uchaguzi huu umefanyika bila ushiriki wa chama cha upinzani cha CHADEMA ambao walisusia uchaguzi kwa madai kwamba walitaka mabadiliko ya sheria za uchaguzi kwanza. - #tanzania #uchaguzi2025 #bbcswahili #samiasuluhuhassan #foryou #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw