Muhoho Kenyatta awarai vijana kuleta mageuzi

  • | Citizen TV
    3,364 views

    Nduguye rais mstafu Uhuru Kenyatta, Muhoho Kenyatta amewataka vijana kusimama imara na kuchukua nafasi za uongozi, akiwarai kutumia teknolojia kuleta mageuzi.

    Akizungumza katika kongamano moja la vijana jijini Mombasa, Muhoho alisema nafasi ya vijana katika uongozi imekuwa finyu licha ya wingi wao.