Wanajeshi wawili wafariki kwenye ajali ya ndege Kwale

  • | Citizen TV
    2,146 views

    Wanajeshi wawili wamefariki kwenye ajali ya ndege ya mafunzo ya kijeshi katika eneo la Ndavaya kaunti ya Kwale. Ndege hiyo aina ya Grob 120A ilianguka katika Kijiji cha Viramboni wadi ya Ndavaya, Kaunti Ndogo ya Kinango.Inasemekana kuwa ndege hiyo ilipata hitilafu za kimitambo katika safari ya mafunzo.Kamishna wa Kaunti ya Kwale Steve Orinde amesema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kilichosababisha ajali hiyo..