Mchuuzi aliyepigwa risasi afanyiwa upasuaji

  • | Citizen TV
    981 views

    Mchuuzi aliyepigwa risasi na polisi katikati ya jiji la Nairobi anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Familia yake baada ya kumtembelea katika chumba cha ICU katika hospitali humo ilieleza kuwa Boniface Mwangi Kariuki yuko katika hali mahututi. Usimamizi wa hospitali ya kenyatta nao ukisema madaktari wanafanya kila wawezalo