Ndege ya B-2: Mshambuliaji asiyeonekana kwenye rada,

  • | BBC Swahili
    3,969 views
    Katika hatua ya kijeshi iliyotikisa ulimwengu, Marekani kwa mara ya kwanza imetumia mabomu mazito ya GBU-57 katika "Operesheni Midnight Hammer", ikitumia ndege saba za kisasa aina ya B-2 Spirit kushambulia vituo vitatu vya nyuklia vya Iran. Mashambulizi hayo dhidi ya Fordow, Natanz na Isfahan yameonyesha kwa mara nyingine uwezo wa kipekee wa ndege ya B-2 mshambuliaji asiyeonekana kwenye rada, mwenye uwezo wa kubeba silaha nzito kwa usahihi mkubwa, na aliyeandaliwa kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya kiwango cha juu kisiri kabisa. Lakini kwanini imetumika B-2 spirit? Huyu hapa Mwandishi wa BBC @frankmavura akitueleza kwa kina. #bbcswahilii #israel #nyuklia #silaha #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw