Hoja yawasilishwa kuwatoa Kindiki na Murkomen kwenye sajili ya mawakili

  • | Citizen TV
    8,510 views

    Baraza la maimamu na wahubiri wa kiisilamu nchini wanamtaka waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen kuondolewa kwenye wizara hiyo kwa kile wanachosema ni kuwa hana uwezo wa kusimamia usalama nchini. Wakati huo huo, hoja imewasilishwa kwa chama cha mawakili nchini LSK kutaka waziri Murkomen na Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki kuondolewa kwenye sajili ya mawakili, kutokana na ukikuaji wa sheria ulioshuhudiwa kwenye maandamano.