Familia ya mgonjwa aliyeuwawa hospitalini Kenyatta yataka majibu

  • | Citizen TV
    1,211 views

    Familia ya Edward Maingi Ndegwa, mgonjwa aliyeuawa katika hospitali ya kitaifa ya Rufaa ya Kenyatta inailaumu hospitali hiyo kwa utepetevu. Mamake Edward Maingi anasema kuwa kifo cha kikatili Cha mwanawe hakingetokea iwapo usimamizi wa hospitali hiyo ungechukua hatua za kuwalinda wagonjwa na kumzuia mshukiwa ambaye anatuhumiwa kwa mauaji mengine asitangamane na wagonjwa wengine. Na kama anavyoarifu Franklin Wallah, Mamake Edward Maingi sasa anataka majibu kutoka kwa usimamizi wa Kenyatta kuhusu vipi mgonjwa anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliruhusiwa kutangamana na wangonjwa wengine.