Maafisa wa polisi waonekana kutokwa na kijasho chembamba wakitoa ushahidi mahakamani

  • | Citizen TV
    9,584 views

    Maafisa wa polisi walionekana kutokwa na kijasho chembamba walipokuwa wakielezea kuhusu silaha walizopewa wakati wa maandamano ya mwaka jana ambapo Rex Kanyike Masai aliuwawa kwa kupigwa risasi. Uchunguzi wa rekodi za usajili wa silaha ulibainisha taarifa zinazotofautiana na ushahidi waliotoa maafisa hao huku wakipata wakati mgumu kuelezea tofauti hizo. Aidha wachunguzi sasa wanatafuta kubaini silaha iliyotumiwa kwenye mauaji ya Rex Masai Juni tarehe ishirini.