Ruto: Elimu ya bure ipo, serikali imejitoa kikamilifu

  • | Citizen TV
    3,664 views

    Rais William Ruto sasa anasema elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari itaendelea kama ilivyokuwa, kinyume na msimamo wa awali wa waziri wa hazina kuu John Mbadi kuhusu kupunguzwa kwa mgao. Rais Ruto akishikilia kuwa elimu ya bure haiwezi kutatizika kwa njia yoyote kwa kile anasema ni uwekezaji wa miundomsingi ya elimu.