Ladha ya amani yarejea Kerio baada ya miaka ya machafuko

  • | Citizen TV
    935 views

    Kwa miongo kadhaa, bonde la Kerio limekuwa na tatizo ya ukosefu wa usalama uliosababisha vifo na hata wakaazi kupoteza mali na makao yao. Wezi wa mifugo kwa miaka walitawala vijiji na kutatiza kabisa maisha na hata shughuli za masomo. Hata hivyo, kwa miaka miwili sasa, hali imeonekana kubadilika baada ya operesheni ya kiusalama iliyoanzishwa mapema mwaka 2023.