Safaricom yajenga hospitali ya milioni 45 Tharaka Nithi

  • | Citizen TV
    238 views

    Kampuni ya Safaricom imeshirikiana na kaunti ya Tharaka Nithi kujenga kituo cha matibabu kitakachokuwa na uwezo wa kuwahudumia kina mama wajawazito 40 katika eneo la chuka igambang'ombe.mradi huo utakaogharimu shilingi milioni 45 unatarajiwa kukamilika chini ya mwaka mmoja ujao. kituo hiki kitakuwa na sehemu mbili za kuwahudumia wagonjwa mahututi pamoja tangi la kuhifadhi gesi ya oksijeni.Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki amesema kituo hicho kitaimarisha huduma za afya kwa kina mama wajawazito huku Safaricom ikiutaja kuwa mchango wake wa kuimarisha huduma kwa wananchi.