Wizara Yapiga Marufuku Kasoro Katika Ajira za Uuguzi

  • | K24 Video
    4 views

    Wizara ya afya leo imewateua wanafunzi watarajali 316 wa shahada ya uuguzi kwa kipindi cha mafunzo kazini. Kulingana na wizara hiyo, hatua hiyo inalenga kurekebisha kasoro zilizoibuka katika awamu ya awali ya usajili. Uamuzi huu unafuatia ukaguzi wa ndani uliobaini mapungufu katika mchakato, ambapo baadhi ya wanafunzi waliohitimu waliondolewa kimakosa, huku wengine ambao hawakuwa wamekamilisha hatua za mwisho za masomo wakijumuishwa.