“Nimeshuhudia Jeshi la Israel likiwafyatulia risasi Wapalestina”

  • | BBC Swahili
    1,725 views
    Afisa wa zamani wa vikosi maalum vya Marekani amefichua kwa BBC sababu ya kujiuzulu kazi yake katika vituo vya usambazaji misaada vya Gaza Humanitarian Foundation (GHF), vinavyoungwa mkono na Marekani na Israel. Anthony Aguilar aliiambia BBC kuwa katika maisha yake yote ya kikazi hajawahi kushuhudia kiwango cha “ukatili na matumizi ya nguvu kupita kiasi na visivyo vya lazima dhidi ya raia wasiokuwa na silaha na wanaokumbwa na njaa.” GHF imeyataja madai yake kuwa “ya uongo kabisa,” huku Jeshi la Ulinzi la Israel likisisitiza kuwa halijawahi kulenga raia. #bbcswahili #gaza #palestina Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw