Maandalizi ya lala salama kwa dimba la CHAN

  • | Citizen TV
    2,797 views

    Wakenya wanasubiri kwa hamu kushabikia timu ya taifa Harambee Stars itakapoingia uwanjani kwa mechi ya kwanza ya dimba la CHAN katika uwanja wa kitaifa Kasarani, Nairobi. Aidha, matayarisho yamekamilika nchini kabla ya mechi za makundi na mchujo zitakazochezwa hapa nchini. Seth Olale na taarifa kamili kuhusu maandalizi ya lala salama.