Mgogoro Mpya Wazuka KEMSA Kufuatia Kesi Dhidi ya Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu

  • | K24 Video
    21 views

    Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa Nchini (KEMSA) imekumbwa na mzozo mpya baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani kupinga uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Waqo Dulacha Ejersa. Mlalamikaji anaitaka Mahakama ya Ajira na Kazi kutangaza uteuzi huo kuwa kinyume cha Katiba, akidai kuwa ulikiuka maadili na sheria za utumishi wa umma. Inadaiwa kuwa Dkt. Waqo alirudi kazini kinyume cha sheria baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.