Unyonyeshaji Wa Maziwa Ya Mama: Tumaini Kwa Watoto Walio Hatarini

  • | K24 Video
    21 views

    Uhusiano wa kipekee kati ya mama na mtoto kupitia unyonyeshaji unaendelea kukumbwa na changamoto nchini Kenya. Huku dunia ikiadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji, takwimu zinaonesha kuwa karibu watoto 4 kati ya 10 bado wanakosa fursa ya kunyonyeshwa. Katika taarifa hii, Eunice Omollo anasimulia safari ya Magdalene Makau, mama ambaye uzoefu wake binafsi ulimchochea kusaidia wengine katika Hospitali ya Pumwani—makao ya benki ya kwanza ya maziwa ya binadamu nchini.