FKF Yafanya msafara wa kutoa hamasa Nairobi

  • | Citizen TV
    893 views

    Shirikisho la Soka Nchini (FKF) limetoa hamasa kwa mashabiki wa soka nchini kuhusu umuhimu wa nidhamu uwanjani wakati wa kipute cha CHAN kinachopigwa katika uwanja wa Kasarani na Nyayo. Kwa ushirikiano na kampuni ya Royal Media Services, FKF Imefanya msafara jijini Nairobi na kusisitiza kuwa maeneo maalum ya kutazama mechi hizo moja kwa moja yametengwa kwa mashabiki ambao hawatapata tiketi za kuingia uwanjani. steve shitera alikuwa kwenye msafara huo na ameandaa taarifa ifuatayo.