- 67 viewsDuration: 1:46Tume ya kupambana na ufisadi hapa nchini EACC, pamoja na washikadau wengine kutoka Afrika mashariki na kusini wa uchunguzi wa ulanguzi wa pesa wamekutana leo Jijini Nairobi kwenye Warsha ya Kanda ya Kushughulikia Ulanguzi wa Pesa na Kurejesha Mali iliyoibwa. Warsha hiyo, inalenga kuimarisha ushirikiano na mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ulanguzi wa fedha.