- 577 viewsDuration: 3:12Zaidi ya watu mia tatu nchini Tanzania sasa wanakabiliwa na shtaka kubwa zaidi katika sheria za nchi hiyo - uhaini. Walioshtakiwa walikamatwa baada ya machafuko yaliyofuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata mwisho wa mwezi uliopita. Miongoni mwao ni wanasiasa, wanaharakati wa mitandao ya kijamii, raia wa kawaida, na hata watoto wadogo walio na umri wa miaka kumi na tatu