Boti ya Uhai: Tegemeo la kuokoa maisha Malawi

  • | BBC Swahili
    815 views
    Kisiwa cha Chisi, nchini Malawi, kinakumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya. Wagonjwa wanalazimika kushindana na muda, wakisafiri kwa zaidi ya saa mbili kuvuka maji kwa mitumbwi dhaifu. Lakini mwaka 2023 mambo yalibadilika baada ya kuletwa kwa “Boti ya Uhai”, inayowaunganisha wakaazi wa kisiwa hicho na huduma za dharura za afya zilizopo nchi kavu, hususan huduma za afya ya kina mama. Katika nchi yenye changamoto za usafiri kama vile barabara mbovu, gharama kubwa au ukosefu wa huduma za magari ya wagonjwa, hali inayochelewesha sana upatikanaji wa matibabu ya dharura, boti hii imekuwa tegemeo la kuokoa maisha. Anne Okumu anaelezea kwa kina #bbcswahili #malawi #afya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw