Raila apinga matokeo ya uchaguzi Kenya

  • | VOA Swahili
    4,310 views
    Kinara wa upinzani Raila Odinga leo amevunja ukimya na kukataa matokeo ya rais yaliyompatia ushindi Naibu rais William Ruto. Katika Mkutano na waandishi wa habari siku moja baada ya matokeo yaliyoonyesha ameshindwa kwa tofauti ndogo, amesema walichokiona jana ni kupuuzwa waziwazi kwa Katiba ya Kenya.