- 136 viewsDuration: 4:35Baadhi ya wakaazi wa Dongo Kundu huko likoni kaunti ya Mombasa wanadai fidia kutoka kwa serikali ili kutoa nafasi ya uwekezaji katika ardhi ya ekari 1000. Kulingana nao, serikali imewanyanyasa na kuafikia fidia duni. Wakazi hao pia wanawalaumu viongozi kwa kukosa kuingilia kati na kuhakikisha wamepewa fidia inayolingana na kiasi cha ardhi wanachomiliki. Baadhi ya wakazi wamepokea fidia ya mradi huo wa eneo maalum la kibiashara.