- 2,253 viewsDuration: 1:15Maafisa wa usalama wa kaunti ya Embu wamewataka wanablogu wanne wa eneo hilo kuandikisha taarifa kuhusiana na vitisho kwa kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua. Kamishna wa kaunti hiyo Jack Obuo, amesema kuwa wanne hao wanahusishwa na madai ya kumtishia Gachagua ambaye amepanga kuzuru eneo hilo kumfanyia kampeni mgombea wa DCP Eneo bunge la Mbeere North, Newton Karish. Wanablogu hao ni pamoja na Simon Njagi Njiru, anayejulikana kama Gikundo wa Gikundo.