- 164 viewsDuration: 2:16Viongozi wa Kiislamu katika Kaunti ya Nandi wanamshinikiza mwenyekiti wa SUPKEM Hassan Ole naado ajiuzulu mara moja. Hii ni baada ya kunaswa kwenye kamera za CCTV akifyatua risasi kuelekea kwa waandamanaji waliokuwa wakipinga uongozi wake. Wakizungumza katika Msikiti wa Jamia, huko Kapsabet, viongozi hao walimtaka Ole naado aondoke ili uchunguzi kamili ufanywe kuhusu tukio. Aidha Viongozi hao pia wametoa wito kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai kuchukua hatua haraka na kuanzisha uchunguzi.