- 8,960 viewsDuration: 2:25Rais William Ruto ametoa agizo kwa idara ya polisi kukabiliana vikali na makundi ya wahuni wanaovuruga amani nchini. Rais ameyasema hayo kwenye mahafali ya Machifu na manaibu wao 1,837 waliofuzu leo baada ya kukamilisha masomo ya utawala, sheria na usalama katika chuo cha mafunzo ya polisi bewa la Embakasi hapa jijini Nairobi.