- 1,824 viewsDuration: 1:19Mwakilishi wadi mteule wa kabuchai kaunti ya bungoma erick wekesa sasa anadai kuandamwa kisiasa kufuatia ushindi wake wa uchaguzi mdogo wa juma lililopita. Wekesa akidai madai ya kuhusishwa na ulaghai wa kahawa katika eneo la tinderet ni ya kutatizwa kuapishwa kwake. Hii inafuatia taarifa ya kumtaka kujisalimisha kaunti ya nandi kwa madai hayo. Mwakilishi wadi huyu mteule pia amekuwa akidai kuwa maisha yake yako hatarini baada ya ushindi huo.