- 1,259 viewsDuration: 2:55Idara ya kupambana na mihadarati nchini itafanyiwa mageuzi na kuongeza idadi ya maafisa ili kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya nchini. Rais William Ruto akimuagiza Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja kuimarisha kitengo hicho kama ilivyopendekezwa kwenye ripoti ya Jukwaa la Usalama aliyokabidhiwa leo na waziri wa usalama Kipchumba Murkomen. Aidha mageuzi mengine yanatarajiwa kuhusu kukabili dhulma za kijinsia na magenge ya wahuni.