- 387 viewsDuration: 1:51Idara ya mahakama imetakiwa kubadilisha mifumo yake ili kuwavutia wakenya wengi kutumia huduma zake. Kwa sasa ni asilima 10 tu ya wakenya ambao wanaenda mahakamani kutafuta haki huku asilimia 19 wakisusia huduma za mahakama. Wengi wa wakenya kwa asilimia 71% wanachagua huduma mbadala za haki. Jaji mkuu Martha Koome na naibu wa Rais Kithure Kindiki sasa wanasema mahakama lazima itafute mbinu nyingine za kuwahudumia wakenya ili kuwawezesha watu wengi zaidi kupata haki. Wamezungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la 22 la majaji na mahakimu wa Afrika mashariki jijini Nairobi.