Skip to main content
Skip to main content

Watu watatu wauawa Ikolomani huku wakazi wakipinga uchimbaji wa dhahabu

  • | Citizen TV
    219 views
    Taharuki imetanda eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega baada ya watu watatu kuuawa kufuatia makabiliano makali kati ya wakazi na polisi. Maafisa wa usalama na wanahabari walijeruhiwa baada ya wakazi waliojawa na hasira kukatiza shughuli ya kupata maoni ya wananchi kuhusiana na mradi wa kuchimba dhahabu ya thamani ya zaidi ya shilingi nusu trilioni. Wenyeji wamepinga mradi huo wakisema hatua hiyo itawalazimu kuhama na kuharibu kipato chao.