- 1,597 viewsDuration: 1:37Mahakama kuu ya Kerugoya imefutilia mbali jopo la wataalamu walioteuliwa na Rais William Ruto kuongoza shughuli ya utoaji fidia kwa waathiriwa wa maandamano dhidi ya serikali. Jaji Edward Muriithi alitoa uamuzi kwamba rais hana mamlaka ya kikatiba kubuni jopo la kutoa ushuri kuhusu utoaji fidia kwa waathiriwa. Mahakama pia ilisema wajibu huo unafaa kutekelezwa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu. Akitoa uamuzi huo, jaji huyo aliagiza hatua zifaazo zichukuliwe katika muda wa siku 30 ili kuendana na katiba. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive