- 12,390 viewsDuration: 2:41Baraza la wanahabari nchini MCK limemshutumu aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake ya kizushi na hatari dhidi ya wanahabari. Kwenye taarifa yake, MCK imeonya kuwa matamshi ya Gachagua ni ya kutishia uhuru wa wanahabari na kuhatarisha maisha yao. Gachagua hivi maajuzi alikosoa vyombo vya habari kwa kile alidai ni kutoa taarifa zisizo kweli kwenye vurumai lililozuka alipokuwa kanisani huko Kariobangi North