- 650 viewsDuration: 1:48Bunge la Kaunti ya Nyamira limekosoa vikali uamuzi wa Seneti kukosa kusikiliza hoja ya kumng’oa Gavana Amos Nyaribo mamlakani, likisema masuala ya msingi yalipuuzwa. Badala ya kuangazia madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka, Seneti ilijadili zaidi hoja ya awali ya mawakili wa Gavana Nyaribo, hatua ambayo Bunge la Kaunti hiyo linadai imewanyima wakazi wa Nyamira haki.