Skip to main content
Skip to main content

Je nani anaamua mipaka ya kujieleza mitandaoni Tanzania?

  • | BBC Swahili
    31,126 views
    Duration: 2:14
    Tanzania imeingia kwenye mvutano mkali kati ya teknolojia na haki za binadamu baada ya Meta, wamiliki wa Instagram na WhatsApp kufuta akaunti za wanaharakati Mange Kimambi na Maria Sarungi. Hatua hii imeibua swali kubwa: je, ni utekelezaji wa sera, au ni juhudi za kuzima sauti za ukosoaji wa serikali? Meta inadai akaunti hizo zilifutwa kwa “kuvunja masharti mara kwa mara,” lakini haijataja machapisho gani hasa yaliyoenda kinyume. Hii inazua maswali: kwa nini hatua hii ilikuja kilele cha mjadala wa maandamano mapya yanayopangwa Desemba tarehe 9? Je, Meta inafanya maamuzi kwa kufata sera na kanuni zao au imepokea shinikizo kutoka kwa serikali ya Tanzania? @mrstadicha anaangazia taarifa hii - - #bbcswahili #tanzania #meta #wanaharakati #mangekimambi #mariasarungi #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw