- 4,172 viewsDuration: 5:02Kenya inaendelea kupoteza maelfu ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, kupitia vifo ambavyo madaktari wanasema vinaweza kuzuilika. Kukosekana kwa vifaa, nafasi finyu, na mifumo duni ya rufaa katika hospitali nyingi za umma kunawafanya watoto njiti kuaga dunia. Huduma maarufu ya kina mama kuwahudumia watoto wa aina hii inaokoa maisha ya watoto hao lakini hospitali nyingi humu nchini hazina nafasi ambazo kina mama hao wanaweza kusaidika