Washukiwa wa shambulizi la shule kaunti ya Samburu wafikishwa mahakamani

  • | Citizen TV
    418 views

    Washukiwa wa shambulizi katika shule ya wasichana ya Kisima Samburu ya Kati kaunti ya Samburu walifikishwa mahakamani mjini Maralal . Wawili hao, Lenolngino Metinda na Mesau Ledunda walishtakiwa kwa kosa la kushambulia shule hiyo ya wasichana ya Kisima mnamo tarehe 24 Septemba mwaka huu na kuiba ng'ombe kumi wenye dhamana ya shilingi milioni moja. Lenolngino na Mesau ni wawili tu miongoni mwa wengine ambao walikamatwa. Watuhumiwawa walikiri mashtaka n akurudishwa kizuizini. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 28 mwezi ujao.