- 14,903 viewsDuration: 3:42Watu 31 wamefariki katika ajali tofauti za barabarani kote nchini katika muda wa saa 24 pekee. Kwenye mikasa ya punde, watu 12 wamefariki kufuatia ajali zilizotokea huko Lugari, Kakamega na Sachangwan, kaunti ya Nakuru. Kwa mujibu wa mamlaka ya usalama barabarani, ajali 17 zimeripotiwa kwa siku moja, huku magari 400 yakinaswa kwa kukosa kuzingatia sheria za usalama.