Papa Leo XIV ameadhimisha Krismasi yake ya kwanza akiwa papa kwa ujumbe wa kuwahimiza Wakristo duniani kote kuwajali maskini, kuwakaribisha wageni na kutetea hadhi ya binadamu.
Alitoa ujumbe huo wakati akiongoza Misa ya Krismasi Jumatano usiku katika Kanisa la St. Peter’s Basilica jijini Vatican. Waumini 6,000, viongozi wakuu wa Kanisa na wanadiplomasia walihudhuria. Nje, watu wengine wapatao 5,000 walifuata Misa kwenye skrini kubwa katika uwanja wa St. Peter's Square, wakivumilia mvua kubwa walipokuwa wakiadhimisha kuzaliwa kwa Kristo.