- 195 viewsDuration: 1:39Wafungwa katika gereza la Lodwar wametakiwa kuwa na nidhamu wanapotumikia kifungu chao huku wakihimizwa kukumbatia elimu na kupata ujuzi wa kiufundi gerezani. Akizungumza alipowatembelea wafungwa hao kusherekea pamoja sherehe za Krisimasi ,gavana wa Turkana Jeremiah Lomorukai amewataka wafungwa watakamaliza kifungo chao wazingatie maadili. Gavana Lomorukai ametoa fahali sita na bidhaa nyingine muhimu kwa wafungwa hao ili kusherekea Krisimasi huku akizindua studio ya muziki itakayowasaidia wafungwa wenye talanta ya muziki