- 8,559 viewsDuration: 2:08Familia ya daktari wa kenya Ambrose Kimiti Mwangi, ambaye alikuwa miongoni mwa kikosi cha madaktari wa Umoja wa Mataifa cha kuwahamisha madaktari nchini Somalia, imetoa wito wa dharura kwa Serikali ya Kenya, Umoja wa Mataifa, Iqarus na washirika wa kimataifa kuzidisha juhudi za kuachiliwa kwake. Hii inafuatia kusambazwa kwa video isiyo na tarehe ambapo Kimiti anasema yeye na timu yake wamekuwa wakizuiliwa na Al-Shabaab tangu Januari 10, 2024, baada ya helikopta yao kutua kwa dharura katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo hao. familia yake inasema majaribio ya kupata taarifa kutoka Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya yamegonga mwamba.