- 572 viewsDuration: 1:31Naibu rais kithure kindiki amewataka madereva na watumizi wengine wa barabara kuwa makini ili kuzuia ajali zinazotokana na utepetevu barabarani. Akizungumza na wakazi wa tharaka nithi pamoja na majirani zao waliofurika nyumbani kwake irunduni kwa sherehe za krismasi, kindiki alisema ingawa serikali inajizatiti kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara nyingi nchini, wasafiri wote wanatakiwa kuzingatia nidhamu na sheria za trafiki ili kuzuia maafa barabarani.